Inatupasa kutumia kila njia iliyo halali kuleta nuru kwa watu. Vyombo vya Habari vitumike, kila shirika la matangazo litakalovuta usikivu juu ya kazi ya Mungu
Ellen G. White, Testimonies to The Church Vol 6.
KUHUSU IDARA YA MAWASILIANO NA VYOMBO VYA HABARI.
Waadventista wanapowasaidia marafiki zao kuelewa Biblia, wanashiriki tumaini ambalo linaweza kupatikana kwa Yesu pekee. Idara ya Mawasiliano husaidia kutoa zana kwa taasisi za kanisa na washiriki kushiriki tumaini hili. Kupitia programu za simu, tovuti, kurasa za mitandao ya kijamii, utayarishaji wa vipindi vya video, sauti, na habari, idara hii hufikia hadhira ndani na nje ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato. Kusudi kuu likiwa ni kutoa njia nzuri na za kukaribisha watu wamjue Yesu.
MKURUGENZI WA IDARA YA MAWASILIANO NA VYOMBO VYA HABARI.

Musa Nathan Mandele alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano katika kikao cha Mkutano Mkuu wa South Nyanza Conference wa Septemba 2022.
Bw Mandele ambaye ni mtaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano amehudumu kama meneja wa TEHAMA wa South Nyanza Conference kuanzia 2015 hadi alipochaguliwa kuongoza idara ya mawasiliano.
Musa Nathan Mandele amehitimu Shahada ya Kwanza ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) mwaka 2013. Alihitimu elimu yake ya juu kutoka Shule ya Sekondari ya Highlands mwaka 2010 na kidato cha nne kutoka Sekondari ya Sadani mwaka 2007.
Alizaliwa mkoani Iringa. Musa Mandele ni mume wa Joyce Mandele ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2018 na kwa sasa wana mtoto wa kiume anayeitwa Davian. Nje ya huduma yake kupitia TEHAMA, Musa Mandele pia ni mkufunzi wa Muziki wa Kikristo aliyehitimu kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) akifurahia kutumia muda wake kuliongoza kanisa katika muziki ufaao kwa ajili ya ibada ya Kikristo.