Siku ya Kwanza: Uko Wapi? (Somo la Watoto)

Jambo Muhimu: Mungu Anataka Kuungana Nasi

Fungu: “BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?”

Mwanzo 3:9

Wazo Kuu

Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, walifurahia wakati pamoja kila siku. Mungu aliwaonya wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Lakini walichagua kumsikiliza nyoka. Adamu na Hawa hawakumtii Mungu na wakaogopa kukutana naye. Walijua kwamba walikuwa wamefanya makosa na walijificha kutoka kwa Mungu. Lakini Mungu aliwapenda, akawaita na kuwauliza “Mko wapi?” Alijua waliko lakini aliwapa nafasi ya kujidhihirisha. Walitoka nje na akawasamehe na kufunika aibu yao.

Muda wa Maombi – Kuombea Moyo Uliounganishwa Upya

Mpendwa Mungu, Baba yetu wa mbinguni, asante kwa kunipenda hata pale nilipokosea. Asante kwa kutokukata tamaa juu yangu. Uliahidi kwamba nikitubu dhambi zangu, Utanisamehe. Tafadhali nipe moyo mpya wa kukupenda zaidi na hamu ya kuwa nawe kila siku. Katika Jina la Yesu, Amina!

Pendekezo la Maombi

Sifa na Shukrani: Toa shukrani kwa baraka maalum na umsifu Mungu kwa wema wake
Kuungama: Ungama makosa yako na umwombe Mungu msamah
Mwongozo: Mwombe Mungu atuweke karibu Naye ili kukuza uhusiano wa kudumu Naye. Muombe akupe uhusiano wa kusamehe, upendo, na kujali na familia, marafiki, majirani, na washiriki wa kanisa.
Kanisa: Ombea uongozi wa kanisa la ulimwengu na washiriki wa kanisa letu wabaki na umoja na kutoa msaada kamili kwa ajili ya utume wa Mungu ili idadi isiyohesabika ibarikiwe na wokovu.
Maombi: Ombea mahitaji ya kiroho kwa wanafamilia wote, marafiki, washiriki wa kanisa, na majirani. Omba kwamba upendo wa Mungu utufafanue na utusogelee karibu Naye na kila mmoja wetu daima. Omba kwamba upendo na kujitolea kwetu kwa Mungu na kila mmoja wetu kukue kila siku.

    1 comments

  • | January 11, 2023 at 7:26 am

    Iko vizuri

Leave a Reply to Paul masolwa Lugandu Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *