Nidhamu Itokanayo na Utii kwa Mungu Hutibu Tamaa

Na Mch E. Kasika

Ndoa haiwezi kuponya tamaa. Kama ndoa ingeliponya tamaa zinaa insingelikuwepo. Kujitawala bado ni hitaji muhimu. Tamaa haijali kuwa una ndoa au hauna. Unaweza kuwa mwenye hekima kama Suleiman, au mpenda kumsifu Mungu kama Daudi, au mwenye imani kama Ibrahim, kiongozi shujaa kama Joshua. Kama hauna nidhamu ya utii kama Yusufu, unaweza ukajikuta unaishia kwenye kuangamizwa kama ilivyotokea kwa Samson. Tusisahau kuwa wote waliotajwa juu walikuwa ni watumishi wa Mungu wenye bidii. Katika hatua fulani ya maisha yao, walijikuta wakisahau ushauri na maagizo kidogo tu kutoka kwa Mungu, kama siyo kwamba hawakumtangaza Muugu wao kwa mshawishi aliyekusudia kuwatoa kwake,ili wamweleze kuwa hawawezi kufanya wanachoshawishiwa naye kufanya wasije wakamkosea Mungu wao.
MAAGIZO YA MUNGU WAKO YAKITAJWA WAZI KWA KILA JARIBU ADUI ATAKUKIMBIA. FANYA HIVYO UUFURAHIE ULINZI WA MUNGU LEO

    2 comments

  • | December 16, 2022 at 10:38 am

    Amen
    Nimebarikiwa na ujumbe huu
    Kama ilivyoandikwa katika kitabu Cha 1 Samweli 15:22 Bwana hupendezwa na utii anasema “….Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,……”

Leave a Reply to Mwl. Mwakalasya Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *