Elimu, Uhuru wa Dini na Mambo ya Kijamii

Kumrudisha binadamu apatane na Mungu, hata kumkuza na kumwadilisha moyoni mwake ili aweze tena kurudisha sura ya Muumbaji, ndilo kusudi kubwa la elimu na malezi yote ya maisha. Hii ilikuwa kazi ya maana sana hata ikamfanya Mwokozi ayaache makao ya mbinguni na kuja ulimwenguni humu katika hali ya mwili wa kibinadamu, Kusudi apate kuwafundisha watu jinsi ya kupata hali ya kufaa kwa maisha yale bora zaidi ya juu.

Kutayarisha Njia 229.4

MKURUGENZI WA IDARA YA ELIMU, UHURU WA DINI & MAMBO YA KIJAMII.


MIONGOZO NA NYARAKA

MUONGOZO WA IDARA YA ELIMU KWA WACHUNGAJI, WAZEE NA VIONGOZI WA ELIMU KANISANI

Mwongozo huu umeandaliwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa elimu ya kikristo kwa washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato na hasa kwa viongozi wanaosimamia idara ya elimu makanisani. Unalenga kutoa ufafanuzi wa idara ya elimu katika ujumla wake ukiwa umeandaliwa na Mchungaji na Mwalimu Marco F. Mlingwa

WAJIBU WA KANISA KWA MTOTO

Muongozo huu muhimu huelezea mambo ambayo kama jumuiya ya waamini tunapaswa kuyafanya kwa ajili ya watoto wetu.