TAMKO LA UTUME WA KANISA
Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ni kuwaalika watu wote wawe wanafunzi wa Yesu, kutangaza Injili ya milele katika muktadha wa Ujumbe wa Malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12, na kuuandaa ulimwengu kwa marejeo ya Kristo yaliyo karibu.
UTEKELEZAJI WA UTUME WETU
Kwa kuongozwa na Biblia na Roho Mtakatifu, Waadventista wa Sabato hutekeleza utume huu kupitia maisha yanayoakisi alivyoishi Kristo, katika kuwasiliana, kufanya wanafunzi, kufundisha, kuponya, na kuhudumia.
NJOZI YA UTUME WETU
Kwa kupatana na mafunuo ya Biblia, Waadventista wa Sabato tunauona utume wetu ukifikia kilele katika mpango wa Mungu wa urejeshwaji wa viumbe vyake katika ukamilifu wa mapenzi yake na haki yake.