
Kanisa la Waadventista wa sabato ni kanisa lenye uongozi wa uwakilishi. Hii inamaanisha washiriki wakiongozwa na Roho wa Mungu ndio wenye uamuzi wa mwisho kuhusu ni nani anayeongoza kanisa. Waumini wa Kiadventista hukusanyika na kuwapigia kura wawakilishi wao katika ngazi ya Kanisa mahalia, Mtaa, Konferensi, Union na General Conference. Wanachama wenyewe, wakiongozwa na Mungu, huchagua viongozi watumishi kwa majukumu yao.

Pr Beatus Greyson Mlozi
Mwenyekiti – South Nyanza Conference
Mchungaji Beatus G Mlozi, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa jimbo la South Nyanza la kanisa la Waadventista Wasabato mnamo Septemba 2022 wakati wa Kikao cha Mkutano Mkuu wa Konferensi jijini mwanza. Alizaliwa Kihesa , Iringa mnamo Machi 23, 1963. Mchungaji Mlozi ambae pia ni mwalimu na mshauri ametumika katika Kanisa la Waadventista wa Sabato kwa takriban miongo mitatu.
Katika kipindi hicho Mchungaji Mlozi amehudumu kama mchungaji wa mtaa katika mitaa ya Lindi, Dodoma, Magomeni na Tabora, mkurugenzi wa idara za uwakili, uchapishaji, na mawasiliano katika konferensi za West Tanzania na South Nyanza na mwenyekiti wa South Nyanza Conference.
Alipata elimu ya theolojia katika chuo kikuu cha Eastern Baraton kampasi ya Arusha, Shahada ya uzamili (Master’s degree) ya Theolojia katika Chuo cha Newbold Uingereza na Masters katika Masuala ya Uongozi kutoka katika Chuo kikuu cha Kiadventista cha Afrika kilichopo Nairobi, Kenya.
Mchungaji Beatus Mlozi na mke wake mama Monica Mlozi, ni wazazi wa watoto watatu, Grace, Ruth na Daniel wakiwa wamebarikiwa na wajukuu wawili Jonathan na Nathanael.

Pr Onesmo Mabula Daniel
Katibu Mkuu – South Nyanza Conference
Baada ya kupata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ibindo, Pr Onesmo aliendelea na kujiunga na Shule ya Sekondari Ihungo kwa ajili ya elimu yake ya upili na baadaye kupata Diploma ya Uchungaji (1991), Shahada ya Kwanza ya Theolojia (2001) na Shahada ya Uzamili ya Theolojia (2014).
Alianza wito wake kama Mwinjilisti wa vitabu chini ya marehemu Pr. Joseph Bohole kabla ya kuwa mchungaji wa wilaya ya Magu, Maswa, Sirari, Mchungaji mlezi katika Sekondari ya Bupandagila, Mkurugenzi wa Huduma za Binafsi na Mkurugenzi wa Shule ya Sabato katika Konferensi ya Nyanza Kusini. Kikao cha 8 cha Konferensi ya Nyanza Kusini kilichoketi Septemba 2022 kilimchagua kuwa katibu mkuu wa Konferensi ya Nyanza Kusini ya Kanisa la Waadventista Wasabato.
Alizaliwa mwaka 1960 katika kijiji cha Mwankuba – Mwanza. Pr Onesmo amemuoa Bi Addah John Henry. Wana watoto watano: Richard Kalindi Onesmo, Hulda Onesmo, Magreth Mageni Onesmo, Kabula Onesmo na Leah Onesmo.

Elder Mwita James Machage
Mhazini Mkuu – South Nyanza Conference
Elder. Mwita J Machage alichaguliwa kuwa mhazini mkuu wa South Nyanza Conference Septemba 2022 wakati wa Kikao cha Mkutano Mkuu wa Konferensi jijini Mwanza.
Mwita alianza kazi yake ndani ya kanisa mwaka 2010 kama Mhasibu wa Shule ya Sekondari Ikizu iliyoko Mara Conference. Pia amewahi kuhudumu kama Mhazini mkuu wa Shule ya Sekondari Nyabihore, Mhazini Msaidizi wa Southern Highlands Conference, Mhazini mkuu wa Shule ya Sekondari ya Waadventista ya Nyanza, Mhasibu na Mratibu wa SunPlus wa South Nyanza Conference na Mhazini Msaidizi wa South Nyanza Conference nafasi aliyoihudumia hadi Juni 2021 ambapo Kamati Kuu Tendaji ya SNC ilimchagua kuwa Mhazini mkuu wa SNC nafasi aliyoihudumia hadi alipochaguliwa mwezi tena Septemba 2022.
Ana Shahada ya Kwanza ya Business Administration katika Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Arusha (UoA) na Shahada ya Uzamili ya Business Administration katika Utawala wa Rasilimali Watu (MBA-HRM) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na sasa anachukua masomo yake ya CPA.
Elder Machage ambae ni mtoto Mchungaji James Machage na Ritha Mwigune alizaliwa tarehe 20 Desemba 1986. Amemuoa Alice Nyekonde na wanandoa hao wamebarikiwa watoto wawili, Devin na Eliab.