Tatizo Moja la Ajabu Kuhusu Fedha

Fedha huhitajika na kila mtu kufanikisha mahitaji ya maisha. Changamoto yake ni huwa haitoshi siku zote. Ukiwa nayo unatamani kuitunza ili iongezeke, bila kuwa tayari kusaidia wahitaji. Kwa kuitunza wengi hujikuta ni wachoyo,waongo, na wezi. Usalama ni kuishi na ulichonacho kwa nidhamu ya kujinyima, ukisaidia wengine. Jiepushe na mikopo mingi itayokuingiza utumwani na hatimaye aibu mbaya. Mungu humlisha asiye nacho, hata kama hakusaidiwa. Mkabidhi Mungu mahitaji yako, usiyapeleke Bank wakati hujui utalipaje.

Imeandaliwa na Mch E. Kasika, Mshauri wa Masuala ya Vijana, Wazazi na Uongozi, +255 764 151 346.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *