Na Elder Winani S. Winani
Lilikuwa ni kusudi la Mwokozi kwamba baada ya Yeye kupaa mbinguni ili kuwa mwombezi wa mwanadamu, wafuasi Wake walipaswa kuendeleza kazi ambayo Alikuwa ameanza. Je, wakala wa kibinadamu haonyeshi shauku maalum katika kutoa nuru ya ujumbe wa injili kwa wale walioketi gizani? Kuna wengine ambao wako tayari kwenda hadi miisho ya dunia ili kupeleka nuru ya ukweli kwa wanadamu, lakini Mungu anadai kwamba kila nafsi inayojua ukweli itafute kuwavuta wengine kuipenda ile kweli. Ikiwa hatuko tayari kutoa dhabihu maalum ili kuokoa roho ambazo ziko tayari kuangamia, tunawezaje kuhesabiwa kuwa wenye kustahili kuingia katika jiji la Mungu?” 9T 103
Si juu ya mhudumu aliyewekwa wakfu pekee, ana jukumu la kwenda kutimiza agizo hili. Kila mtu ambaye amempokea Kristo ameitwa kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wenzake.” AA 110.
Tabia halisi ya kanisa inapimwa, si kwa kazi ya juu inayofanya, si kwa majina yaliyoandikwa katika kitabu cha kanisa, bali kwa yale ambayo kwa hakika inamfanyia Bwana, kwa idadi ya watenda kazi wake waaminifu na wavumilivu. Kupendezwa kwa kibinafsi, na kukesha, jitihada ya mtu binafsi itatimiza mengi kwa ajili ya kazi ya Kristo kuliko yawezayo kufanywa na mahubiri au kanuni za imani.— The Review and Herald, Septemba 6, 1881.
Akina kaka na dada katika imani, je, swali linatokea mioyoni mwenu, “Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” Ikiwa unadai kuwa watoto wa Mungu, wewe ni mlinzi wa ndugu yako. Bwana analiweka kanisa kuwa na daraka kwa ajili ya roho za wale ambao wanaweza kuwa njia ya kuokoa.— Historical Sketches, 291.
Hiki ni kipindi Cha kufanya uamsho na matengenezo ili kutimiza agizo la Bwana YESU linalosema;”Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.’Mathayo 28:19,20.