Vijana, Chaplensia na Muziki

KUHUSU IDARA YA VIJANA, CHAPLENSIA NA MUZIKI

Vijana na wakumbuke kwamba wanapaswa kujenga tabia kwa ajili ya umilele, na kwamba Mungu anawahitaji wafanye kwa ubora zaidi. Wale walio na uzoefu mkubwa zaidi wawachunge walio wachanga zaidi; na wanapowaona wamejaribiwa, wawaweke kando, na waombe nao na kuombe kwa ajili yao.

Ellen G White, Mashauri kwa Vijana.

Vijana wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato wanathaminiwa sio tu kama kanisa la wakati ujao bali kama wanajumuiya muhimu sana wa kanisa la wakati huu. Idara hii muhimu husaidia kuandaa miongozo na programu mbalimbali ili kusaidia na kuwashauri vijana. Idara hii pia kupitia huduma za chaplensia husimamia utoaji wa mahitaji mbalimbali ya kiroho kwa makundi mbalimbali ya watu kama wanafunzi, wanajeshi na kadhalika.


MKURUGENZI WA IDARA YA VIJANA, CHAPLENSIA NA MUZIKI

Mwalimu Isaacs SYD Manyonyi ana Shahada ya Uzamili ya Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Afrika na Shahada ya Kwanza ya Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwl Manyonyi ana uzoefu wa muda mrefu na historia ya kufanya kazi na vijana. Hapo awali aliwahi kuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Parane na Mwalimu Mkuu katika Shule ya Giti English Medium na Shule ya Sekondari Chome. Amehudumu kama Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Mambo ya Kijamii, Uhuru wa Dini, Vijana, na Muziki katika Konferensi za NETC na SNC.

Mwl Manyonyi ni mume wa Debora Manyonyi, na wamejaliwa watoto wawili wa kike na wawili wa kiume.