Uwakili, Amana na Majengo

KUHUSU IDARA YA UWAKILI, AMANA NA MAJENGO.

Mungu mwenyewe ameanzisha mpango wa kuendesha kazi yake na amewagawia watu wake mazidio ya mali ili wito unapotolewa watoe kwa furaha. Ikiwa watakuwa waaminifu kuleta kwa hazina yake mali ile waliyoazimwa, kazi yake itaendelea upesi. Watu wengi wataletwa kwenye kweli, na siku ya kuja kwa Yesu itaharakishwa.

Ellen G. White, Mashauri Juu ya Uwakili.

Uwakili huhusisha jinsi sisi kama wanadamu tunatunza rasilimali ambazo Mungu ametupatia. Matumizi ya hekima ya kile tulicho nacho husaidia kazi ya Mungu kusitawi na watu wengi zaidi wanaweza kuelewa Biblia na kupata uhuru, uponyaji na tumaini katika Yesu. Idara ya Uwakili husaidia kutoa mafunzo kwa viongozi na washiriki wa Waadventista ulimwenguni kote katika kanuni za uwakili wa kibiblia.


MKURUGENZI WA IDARA YA UWAKILI, AMANA, MAJENGO & ATAPE

Baraka Boniphace Nchama alianza kazi ya utumishi ndani ya kanisa kama mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Nyabihore iliyopo mkoani mara baada ya kuhitimu masomo yake ya Shahada ya Sanaa na Elimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka 2012.

Mwaka 2014 alijiunga na kazi ya Uchungaji ambapo alihudumu katika mtaa wa Mbugani (Geita) na Nyegezi na baadaye Mkurugenzi wa Idara Idara ya Uwakili.

Alihitimu shahada ya uzamili (Master of Divinity) kutoka Chuo Kikuu cha Waadventista cha Afrika (AUA) mnamo 2021.

Amemuoa Jackline Baraka na wana watoto watatu, mabinti wawili: Anaiah na Pelaiah na mtoto mmoja wa kiume: Pedaiah.