Uchapishaji

Maneno ya ujumbe niliyopewa kwa ajili ya watu mbalimbali mara nyingi nimeyaandika kwa faida yao nikifanya hivi kwa wengi wao walionisihi sana kuwafanyia vile. Kadiri kazi yangu ilivyozidi, hili likawa jambo kubwa na sehemu ya kunichosna ya kazi yangu.

Kutayarisha Njia 105.4

Kazi ya uchapishaji, ilianzishwa na James na Ellen White kabla ya Kanisa la Waadventista Wasabato kuwa na jina, ilikusudiwa kuwa na jukumu kubwa katika kutoa injili ya milele kwa ulimwengu katika maandalizi kwa ajili ya ujio wa pili wa Yesu Kristo. Idara hii huratibu kazi ya jumla ya uchapishaji ya kanisa katika South Nyanza. Inatumika kama kituo cha rasilimali katika uzalishaji na usambazaji wa vitabu mbalimbali na tafsiri za vitabu vya Ellen G White.