Kama tukinia tunaweza kufanya kazi nzuri kwa ajili ya Mungu. Mwanamke hajui nguvu zake kwa Mungu. . . . Kuna kusudi la juu kwa mwanamke, hatima kuu. Anapaswa kukuza na kusitawisha nguvu zake, kwani Mungu anaweza kuzitumia katika kazi kubwa ya kuokoa roho kutoka kwenye uharibifu wa milele.
Ellen G. White, Testimonies to the Church Vol 4.
KUHUSU IDARA YA WANAWAKE NA WATOTO
Wanawake hutumika kama sehemu muhimu sana katika Kanisa la Waadventista Wasabato. Mahitaji yao ya kiroho, kihisia, kimwili na kijamii ni muhimu sana. Idara ya Huduma za Wanawake na Watoto inasimamia programu zinazowasaidia wanawake kufikia uwezo wao kamili kama viongozi katika nyumba zao na jamii. Idara hii pia inasimamia mipango ya kukuza ustawi na maendeleo ya watoto kutengeneza nyenzo zinazoendana na umri wao ili kushiriki Biblia na watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka kumi na minne. Wanapojifunza kutoka katika Biblia, mara nyingi watoto huwa wa kwanza kuukubali upendo wa Yesu na kutaka kuwaeleza wengine.
MKURUGENZI WA IDARA YA WANAWAKE NA WATOTO

Martha Zacharia Costantine alichaguliwa katika kikao cha mkutano mkuu wa 2022 kuwa mkurugenzi wa idara ya Wanawake na Watoto na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha AWM-VTC, Pasiansi – Mwanza. Ametumikia kanisa katika nafasi mbalimbali kama mwinjilisti wa vitabu, Meneja wa ABC, APDD wa Kanda, Mkurugenzi wa Idara na Mkuu wa Chuo katika AWM – VTC. Mama Martha amesoma katika Shule ya Msingi Badugu, Shule ya Sekondari Bwasi, Singida VTC, VETA Mwanza na Chuo cha Waadventista Tanzania (Kwa sasa Chuo Kikuu cha Arusha).
Kwa sasa anaendelea na mafunzo ya Uchungaji ngazi ya III katika chuo kikuu cha Arusha. Alizaliwa huko Geita, mzaliwa wa nne wa familia ya Mzee John Isaac Lyabalimi na mkewe Hulda Tagili. Alifunga ndoa Julai 1984 na Zacharia Costantine Mwizalubi na Mungu amewajalia watoto watano.