Yesu aliwaita wanafunzi wake ili awazoeze na kuwafunza ili baadaye awatume ulimwenguni kutangaza mambo yale waliyoyaona na kusikia kwake. Madaraka waliyopewa yalikuwa muhimu sana ambayo watu hawajapewa kama hayo. Madaraka yao yalikuwa ya pili kwa yale ya Kristo mwenyewe. Kazi yao ilikuwa kushirikiana na Mungu ili kuuokoa ulimwengu.
Tumaini la Vizazi Vyote 158.4
Kuhusu Idara ya Huduma Za Kichungaji na Familia
Wachungaji ni watu wenye shughuli nyingi. Wanafanya kazi nyingi muhimu sana kuhudumia jamii zetu. Idara ya Huduma za Kichungaji husaidia kuandaa wachungaji, familia zao na viongozi wao wa mitaa na makanisa na kuwasaidia katika kuhudumia mahitaji ya makutaniko yao na kwa kuwa waadventista wa sabato ni waumini wakubwa wa maisha ya familia yenye furaha, Idara hii pia imejumuishwa na huduma za familia. Hii hulifanya kanisa kuimarisha familia kupitia huduma kama vile miongozo kabla ya ndoa, semina za ndoa, mafunzo kwa wazazi, na elimu maalum ya Biblia inayolenga familia.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kichungaji na Familia

Mchungaji Marco Barnabas Itima alizaliwa June 28,1965 katika mkoa wa Mwanza Wilaya ya Kwimba Kijiji cha Ng’hundya kata ya Bungulwa, mzaliwa wa kwanza wa Mzee Barnabas Kanyasu na Bi Letisia Lugwisha waliokua waumini wa Kanisa la Roman Catholic. Mchungaji Barnabas alipokea imani ya Waadventista wa Sabato mwaka 1985 na kubatizwa June 24,1986 na mchungaji Ayubu Ndulu.
Novemba 14,1990 alifunga ndoa na Ellen Tumaini Kamba katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Malili – Busega na hadi sasa wamejaliwa watoto 6. Pendo, Emmanuel, Kulwa, Dotto, Hulda na Barnabas.
Mchungaji Barnabas alijiunga na Chuo cha Tanzania Adventist College 2001 (kwa sasa University of Arusha), mwaka 2006 alihitimu shahada ya kwanza ya uchungaji. Alianza rasmi huduma ya kichungaji Juni 2006 kama mchungaji wa mtaa wa Nyakato-Mwanza kisha Ntuzu-Simiyu na Shinyanga. Amehudumu pia kama mkurugenzi wa Huduma Binafsi na Shule ya Sabato-SNC na Mwenyekiti wa Tanzania Rift Valley Field.
Mchungaji Barnabas aliwekwa wakfu kwa kuwekewa mikono ya uchungaji March 17,2012.