Idara

Kazi ya Mungu katika jimbo la South Nyanza imegawanywa katika idara na vitengo kadhaa ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu wa Mungu katika maeneo yetu. Lengo kuu la idara zote hizi ni kuutimiza vyema utume wa Waadventista wa kusaidia kila mtu kuelewa Biblia na kupata uhuru, uponyaji na matumaini katika Yesu Kristo.

Idara za South Nyanza Conference

Huduma za Kichungaji na Familia

Wachungaji ni watu wenye shughuli nyingi. Wanafanya kazi nyingi muhimu sana kuhudumia jamii zetu. Idara ya Huduma za Kichungaji husaidia kuandaa wachungaji, familia zao na viongozi wao wa mitaa na makanisa na kuwasaidia katika kuhudumia mahitaji ya makutaniko yao na kwa kuwa waadventista wa sabato ni waumini wakubwa wa maisha ya familia yenye furaha, Idara hii pia imejumuishwa na huduma za familia. Hii hulifanya kanisa kuimarisha familia kupitia huduma kama vile miongozo kabla ya ndoa, semina za ndoa, mafunzo kwa wazazi, na elimu maalum ya Biblia inayolenga familia.

Tazama Zaidi

Uwakili, Amana na Majengo

Uwakili katika upana wake huusisha jinsi sisi kama wanadamu tunavyotunza rasilimali ambazo Mungu anatupa. Matumizi ya hekima ya kile tulicho nacho inamaanisha kwamba kazi ya Mungu inaweza kusitawi na watu wengi zaidi wanaweza kuelewa Biblia ili kupata uhuru, uponyaji na tumaini katika Yesu. Idara ya Uwakili husaidia kutoa mafunzo kwa viongozi na waumini Waadventista ulimwenguni kote katika kanuni za uwakili wa kibiblia. Pia idara hii kupitia huduma za amana hutoa msaada kwa washiriki wa kanisa wanaotaka kusaidia Kanisa kupitia amana na karama zingine maalum. Ikiwa washiriki wanahitaji mwongozo wa kitaalamu wa kifedha, mali na upangaji majengo, idara hii iko hapa kusaidia.

Tazama Zaidi

Huduma Binafsi na Shule Sabato

Mojawapo ya njia bora za kusoma Biblia na kupata uhuru, uponyaji na matumaini katika Yesu ni kujumuika na vikundi vidogo vya watu ambao pia wana nia ya dhati ya kukuza ujuzi wao wa Biblia. Idara ya Shule ya Sabato na Huduma Binafsi hutoa miongozo ya kujifunza Biblia na nyenzo kwa vikundi vidogo vinavyokutana Jumamosi asubuhi na nyakati nyinginezo za juma kujifunza. Haijalishi una umri gani, idara hii ina nyenzo za kukusaidia kumjua Mungu vizuri zaidi na kushiriki mambo unayojifunza na wengine.

Tazama Zaidi

Uchapishaji

Idara ya Huduma za Uchapishaji ya Nyanza Kusini inaratibu kazi ya jumla ya uchapishaji ya Kanisa kwa eneo letu la Utume. Inasimama kama mratibu wa uzalishaji na usambazaji wa vitabu mbalimbali vya kanisa kwa kupitia maduka ya vitabu na wainjilisti wa vitabu.

Tazama Zaidi

Afya na Kiasi

Kusudi kuu la Idara ya Afya na Kiasi ni kuleta uponyaji wa kimwili na wa kiroho kwa watu wa eneo la South Nyanza Conference. Moja ya sababu za Waadventista Wasabato kuishi muda mrefu zaidi kuliko makundi mengine ya watu ni mtindo wao wa maisha. Idara ya Afya hutoa taarifa na mafunzo sahihi kuhusu jinsi ya kuboresha afya yako na kuwa vile ambayo Mungu amekuumba uwe. Mafundisho yake hukusaidia kugundua kile ambacho Biblia inasema kuhusu afya na umuhimu wake katika kuishi maisha yenye mbaraka.

Tazama Zaidi

Vijana, Chaplensia na Muziki.

Vijana wa Kanisa la Waadventista Wasabato wanathaminiwa sio tu kama kizazi kijacho bali pia kama watu muhimu sana kwa kanisa kwa wakati huu. Idara hii husaidia kusimamia miongozo na programu mbalimbali ili kusaidia vijana kuishi kufikia kusudi la Mungu kwa ajili yao.

Tazama Zaidi

Mawasiliano, Satelaiti na Vyombo vya Habari

Waadventista wanapowasaidia marafiki zao kuelewa Biblia, wanashiriki tumaini ambalo linapatikana kwa Yesu pekee. Idara hii husaidia kuandaa zana zinazotumiwa na makanisa na washiriki kusambaza tumaini hili. Kwa njia ya programu za simu, tovuti, mitandao ya kijamii, utayarishaji wa vipindi vya runinga hadi taarifa za habari zinazofikia hadhira ndani na nje ya Kanisa. Kusudi ni kutoa njia nyingi na nzuri za kukaribisha watu wamjue Yesu.

Tazama Zaidi

Wanawake na Watoto

Dhumuni kuu la huduma za wanawake na watoto ni kulea na kuwezesha wanawake na watoto katika maisha yao ya Kikristo kama wanafunzi wa Yesu Kristo na washiriki wa Kanisa lake ulimwenguni. Kwa kushirikiana na idara nyingine za South Nyanza Conference, idara hii inashiriki jukumu la kuandaa mikakati ya kiinjilisti na kutoa mafunzo ya kuwaandaa wanawake na watoto wa kanisa ili kumwinua Kristo katika Kanisa na ulimwengu.

Tazama Zaidi

Elimu, Uhuru wa Dini na Mambo ya Kijamii

Waadventista Wa Sabato wanaamini kwamba kupata elimu kamili ya Kikristo ni njia nzuri ya kumpenda Yesu na kujiandaa kwa maisha ya huduma. Kwa kuzingatia hilo idara hii pamoja na mambo mengine, ina jukumu kuu la kuhakikisha taasisi za elimu za Waadventista zinavuka matarajio na kutoa mwanzo mzuri wa maisha ya wanafunzi wanapita katika shule hizo.

Tazama Zaidi