Kutoka kwenye kalamu za watumishi mbalimbali wa Bwana, mahali hapa pamekusudiwa kuwa na mkusanyiko wa Mawazo, Mafunzo na Jumbe mbalimbali kutoka wachungaji, wazee, watumishi na washiriki kutoka ndani na nje ya konferensi yetu.
Chukizo la Uharibifu Huenda Sambamba na Hukumu ya Upelelezi
Watu wengi wanaofuatilia kutimia kwa unabii, hutumia muda mrefu na kwa makini kufuatilia jinsi unabii wa Ufunuo 13:11-18 unavyotimia haraka. Wafuatiliaji wa karibu wa matukio,hupenda kuonyesha na picha za ushahidi wa viasharia. Hili ni jambo zuri lakini halitakiwi liwe ndilo kipaumbele chetu. Kwa nini? Baada ya unabii wa siku 2,300 wa Daniel 8:13,14, kumalizika mwaka…
Read MoreMatendo ya Mwili Huathiri Mahusiano
Mioyo iliyovunjika haiwezi kutiwa moyo na nyuso zilizokasirika au na sauti kali isiyo na upole au huruma. Watu wenye mawazo mengi na waliokata tamaa hawasaidiwi kurejesha matumaini na mtu aliye mbali, akidai kuwa anawaombea Mungu awasaidie. Kufariji hudhihirishwa na kujali kwa matendo mema yaonyeshayo huruma. Ni kweli kuwa maombi husaidia, lakini uwepo wa mfariji unaongeza…
Read MoreTatizo Moja la Ajabu Kuhusu Fedha
Fedha huhitajika na kila mtu kufanikisha mahitaji ya maisha. Changamoto yake ni huwa haitoshi siku zote. Ukiwa nayo unatamani kuitunza ili iongezeke, bila kuwa tayari kusaidia wahitaji. Kwa kuitunza wengi hujikuta ni wachoyo,waongo, na wezi. Usalama ni kuishi na ulichonacho kwa nidhamu ya kujinyima, ukisaidia wengine. Jiepushe na mikopo mingi itayokuingiza utumwani na hatimaye aibu…
Read More