Wazo Kuu
Mfalme mwovu Ahabu na mkewe Yezebeli walitawala Israeli. Kwa sababu ya mvuto wao mbaya, watu wengi katika Israel walimsahau Mungu na kupuuza ibada. Mungu alimwita nabii Eliya kujenga upya madhabahu zilizovunjika. Eliya alipojenga upya madhabahu, alikuwa akiwaonyesha watu uhitaji wa kujenga upya uhusiano wao na Mungu na kumrudia. Eliya aliwakumbusha watu warudi kumwabudu Mungu wa kweli.
Jenga upya-Atakuja tena
Mpendwa Mungu, Baba yetu wa mbinguni, asante kwa kunipenda hata ninapokosea. Huniacha kamwe na Unaniita nirudi Kwako. Nipe moyo mpya na hamu ya kutaka kuwa na wakati wa pekee na Wewe. Nisaidie niamue kukuabudu kila siku. Katika Jina la Yesu, Amina.
Mapendekezo ya maombi
Sifa na Shukrani: Toa shukrani kwa baraka maalum na umsifu Mungu kwa wema wake
Kuungama: Ungama makosa yako na umwombe Mungu msamaha
Mwongozo: Mwombe Mungu hekima ya kufanya maamuzi yanayofaa
Kanisa: Ombea kanisa la ulimwengu na nchi yetu
Maombi: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia na majirani
Tumsifu Mungu
76 Nataka niwe tayari
95 Niwe kama Yesu
250 Yesu anataka niwe kianga
107 Omba sana asubuhi