Siku ya Pili: Kuweka Wakfu na Ukumbusho (Watoto)

Wazo Kuu

Madhabahu daima zimewakilisha mahali pa kujitolea na ukumbusho. Ni ishara ya uhusiano binafsi na Mungu. Mungu alimwahidi Abrahamu kwamba angekuwa baba wa watoto wengi na kwamba angewapa wazao wake Nchi ya Kanaani. Ili kumheshimu na kumwabudu Mungu, Abrahamu alijenga madhabahu. Ahadi hii na tendo la ibada lilipitishwa kwa mwana wa Abrahamu, Isaka na pia kwa mjukuu wake Yakobo.
Kupitia mifano yao, Waisraeli walijenga madhabahu ili kumheshimu na kumwabudu Mungu. Pia tunakumbushwa kumwabudu na kuzungumza na Mungu kila siku.

Saa ya Maombi

Mahali pa Kukumbuka
Mungu mpendwa, Baba yetu wa mbinguni, asante
kwa yote uliyonitendea. Nataka kukupa heshima, sifa
na ibada. Nisaidie kukumbuka upendo na wema
wako na kuanzia sasa na kuendelea nikuabudu
Wewe kila siku. Katika Jina la Yesu, naomba, Amina

Mapendekezo ya Maombi

Sifa na Shukrani: Toa shukrani kwa baraka maalum na umsifu Mungu kwa wema wake
Kuungama: Ungama makosa yako na umwombe Mungu msamaha
Mwongozo: Mwombe Mungu hekima ya kufanya maamuzi yanayofaa
Kanisa: Ombea watoto na familia zote za SDA kumtafuta Mungu, kumweka Yeye kwanza katika maisha yao, na kumfuata.
Maombi: Ombea Roho Mtakatifu aongoze katika kufanya maamuzi ya watoto wote na kubarikiwa na uchaguzi wao katika kufuata kwa uchangamfu amri za Mungu.

Msifu Mungu

  • 142 Tunamwimbia Mwokozi
  • 139 Nina furaha tele
  • 125 Mungu anajali
  • 56 Msifu Mungu Ee Watoto wote
Nyimbo Zote kutoka Kitabu cha Nyimbo za Kristo za Watoto

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *