
Kama tungelipiza visasi kwa kuwachafua waliotuchafua, kama tungewaharibia waliotuharibia ili kukabiliana nao, Mungu ajuaye yote akiamua kunyanza bila kufunua ni salama? Kuna nguvu katika kukubali aibu, katika kusamehe, katika kukaa kimya, kukubali kudhulumiwa vilivyo vyetu. Kuna nguvu zaidi katika kusimama na Mungu wakati wote. (Mwanzo 45)