Tujifunze Kutoka kwa Yohana na Yuda

Nasaha za Kalamu Iliyovuviwa July 26, 2023

“Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.” 1Yohana 2:6

Yohana na Yuda ni wawakilishi wa wale wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo. Wanafunzi hawa wote wawili walikuwa na fursa sawa za kujifunza na kufuata Kielelezo cha Mungu. Wote wawili walishirikiana kwa ukaribu na Yesu na walikuwa na pendeleo la kusikiliza mafundisho Yake. Kila mmoja alikuwa na kasoro kubwa za tabia; na kila mmoja alikuwa na ufikiaji wa neema ya kimungu ambayo inabadilisha tabia. Lakini wakati mmoja katika unyenyekevu alikuwa akijifunza juu ya Yesu, yule mwingine alifunua kwamba yeye hakuwa mtendaji wa neno, bali msikiaji tu. Mmoja, kila siku akifa kwa nafsi yake na kushinda dhambi, alitakaswa kwa njia ya ukweli; yule mwingine, akipinga nguvu ya neema igeuzayo na kuendekeza tamaa za ubinafsi, aliwekwa katika utumwa wa Shetani……

Kubadilika kwa tabia kama inavyoonekana katika maisha ya Yohana daima ni matokeo ya ushirika na Kristo. Kunaweza kuwa na kasoro kubwa katika tabia ya mtu binafsi, lakini anapofanyika kuwa mfuasi wa kweli wa Kristo, nguvu ya neema ya Mungu humbadilisha na kumtakasa. akiutazama kama katika kioo utukufu wa Bwana, anabadilishwa kutoka utukufu hadi utukufu, hata awe kama yeye ambaye yeye huabudu.” CC 557-559.

Bwana Yesu anasema:
“Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”Ufunuo 3:19,20

BWANA ATUBARIKI NA KUTUTIA NGUVU TUNAPOZIDI KUTAFAKARI NENO LAKE WIKI HII
Nukuu hizi za Roho ya Unabii zimekusanywa na kuwekwa pamoja na Elder Winani S. Winani

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *